Deuteronomy 12:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Bali mtakwenda mahali ambapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atachagua katika makabila yote ili kuliweka jina lake na makao yake hapo; huko ndiko mtakakokwenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bali mtatafuta mahali Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini mahali atakapochagua Bwana, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Bali mtakwenda mahali ambapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atachagua katika makabila yote ili kuliweka jina lake na makao yake hapo; huko ndiko mtakakokwenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bali mtatafuta mahali BWANA Mungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bali mtatafuta mahali bwana Mwenyezi Mungu wenu atakapopachagua katika makabila yenu yote ili aliweke jina lake huko kuwa makao yake. Mahali hapo ndipo iwapasapo kwenda;
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika makabila yenu yote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe uende huko;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Bali mtakwenda mahali ambapo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atachagua katika makabila yote ili kuliweka jina lake na makao yake hapo; huko ndiko mtakakokwenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ila mahali pale pamoja, Bwana Mungu wenu atakapopachagua katika mashina yote pa kuliwekea Jina lake, likae papo hapo, ndipo papasapo, mpaingie mtakapomtafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini mahali atakapochagua BWANA, Mungu wenu, katika kabila zenu zote, apaweke jina lake, maana, ni makao yake, elekezeni nyuso zenu hapo, nawe wende huko;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini mutakwenda pahali ambapo Yawe, Mungu wenu, atachagua katika makabila yote kwa kuweka jina lake na makao yake hapo. Huko ndiko mutakakokwenda.