Deuteronomy 13:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tembeeni kwa kumfuata Bwana, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni BWANA Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni bwana Mwenyezi Mungu wenu ambaye mnapaswa kumfuata tena ni yeye mnapaswa kumheshimu. Shikeni maagizo yake na kumtii, mtumikieni na kushikamana naye.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mfuateni na kumcha Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, na kushika amri zake na kuitii sauti yake; mtumikieni na kuambatana naye.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mfuateni Bwana Mungu wenu na kumcha, myashike maagizo yake na kuisikia sauti yake, mmtumikie na kugandamana naye!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tembeeni kwa kumfuata BWANA, Mungu wenu; mcheni na kushika maagizo yake na kuisikia sauti yake, nanyi mtumikieni na kushikamana naye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
musisikilize maneno ya nabii huyo au mutabiri wa kutumia ndoto, kwa maana Yawe, Mungu wenu, anawatumia kwa kuwajaribu kusudi ajue kama munamupenda yeye Yawe, Mungu wenu, kwa moyo wenu wote na roho yenu yote.