Deuteronomy 13:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ikiwa ndugu yako wa tumbo moja, au mtoto wako wa kiume au wa kike, au mke wako umpendaye sana, au rafiki yako mwandani, atakushawishi kwa siri akisema, ‘Twende tukaabudu miungu mingine’, miungu ambayo wewe wala babu zenu hamuijui,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu,
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ikiwa ndugu yako wa tumbo moja, au mtoto wako wa kiume au wa kike, au mke wako umpendaye sana, au rafiki yako mwandani, atakushawishi kwa siri akisema, ‘Twende tukaabudu miungu mingine’, miungu ambayo wewe wala babu zenu hamuijui,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ndugu yako hasa, au mwanao au binti yako, au mke umpendaye, au rafiki yako wa karibu sana akikushawishi kwa siri, akisema, “Na twende tukaabudu miungu mingine” (miungu ambayo ninyi wala baba zenu hamkuifahamu,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mama yako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ikiwa ndugu yako wa tumbo moja, au mtoto wako wa kiume au wa kike, au mke wako umpendaye sana, au rafiki yako mwandani, atakushawishi kwa siri akisema, ‘Twende tukaabudu miungu mingine’, miungu ambayo wewe wala babu zenu hamuijui,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa, ndugu yako aliyezaliwa na mama yako au mwanao wa kiume au wa kike au mkeo anayekaa kfuani pako au mwenzako, unayempenda, kama unavyojipenda mwenyewe, akuhimize penye njama kwamba: Twende, tutumikie miungu mingine, usiyoijua wewe, wasiyoijua nao baba zako!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Atakapokushawishi kwa siri ndugu yako, mwana wa mamaako, au mwana wako, au binti yako, au mke wa kifuani mwako, au rafiki yako aliye kama moyo wako, akikuambia, Twende tukaabudu miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini nabii huyo au mutabiri wa kutumia ndoto atauawa, kwa sababu atakuwa amewafundisha uasi mbele ya Yawe, Mungu wenu, aliyewatoa katika inchi ya Misri na kuwakomboa kutoka katika utumwa, kusudi muache njia ambayo Yawe, Mungu wenu, aliwaamuru kufuata. Hivi ndivyo mutakavyokomesha uovu kati yenu.