Deuteronomy 14:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nyinyi ni watu watakatifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; Mwenyezi-Mungu amewachagua muwe watu wake hasa, kati ya watu wote waishio duniani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
kwa kuwa ninyi ni taifa takatifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Mwenyezi Mungu amewachagua ninyi kuwa taifa lake la pekee kutoka mataifa yote duniani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako, na Bwana amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nyinyi ni watu watakatifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; Mwenyezi-Mungu amewachagua muwe watu wake hasa, kati ya watu wote waishio duniani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwa BWANA Mungu wenu. BWANA amewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
kwa maana ninyi ni taifa takatifu kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu. bwana amewachagua ninyi kuwa taifa la kipekee kutoka mataifa yote juu ya uso wa dunia, mwe tunu yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, na BWANA amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nyinyi ni watu watakatifu kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu; Mwenyezi-Mungu amewachagua muwe watu wake hasa, kati ya watu wote waishio duniani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani ninyi m watu watakatifu wa Bwana Mungu wako, maana Bwana akikuchagua kuwa kabila lililo lake mwenyewe kuliko makabila yote yakaayo huku nchini.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako, na BWANA amekuchagua kuwa watu wake hasa, kuliko mataifa yote yaliyo juu ya uso wa nchi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ninyi ni watakatifu wa Yawe, Mungu wenu. Yawe amewachagua ninyi kuwa watu wake kati ya watu wote katika dunia yote.