Deuteronomy 14:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Msile nyamafu yoyote; mnaweza kumpa mgeni anayeishi katika miji yenu, ale, au mnaweza kumwuzia mtu wa taifa lingine, kwa sababu nyinyi ni watakatifu na Mwenyezi-Mungu ni Mungu wenu. Msimchemshe mwanambuzi katika maziwa ya mama yake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu. Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa Bwana, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Msile nyamafu yoyote; mnaweza kumpa mgeni anayeishi katika miji yenu, ale, au mnaweza kumwuzia mtu wa taifa lingine, kwa sababu nyinyi ni watakatifu na Mwenyezi-Mungu ni Mungu wenu. Msimchemshe mwanambuzi katika maziwa ya mama yake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msile kitu cho chote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni ye yote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa BWANA Mungu wenu. Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msile kitu chochote mtakachokuta kimekufa. Mnaweza kumpa mgeni yeyote anayeishi katika mojawapo ya miji yenu, naye anaweza kula au mnaweza kumuuzia mtu wa nchi nyingine. Lakini ninyi ni watu watakatifu kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu. Msitokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Msile nyamafu yoyote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumlisha mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Msile nyamafu yoyote; mnaweza kumpa mgeni anayeishi katika miji yenu, ale, au mnaweza kumwuzia mtu wa taifa lingine, kwa sababu nyinyi ni watakatifu na Mwenyezi-Mungu ni Mungu wenu. Msimchemshe mwanambuzi katika maziwa ya mama yake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Msile kibudu cho chote! Mgeni aliomo malangoni mwako utampa, ale, au utakiuza kwa mtu wa kimizimu. Kwani ninyi m watu watakatifu wa Bwana Mungu wenu. Kitoto cha mbuzi usikipike katika maziwa ya mama yake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Msile nyamafu yo yote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikule nyamafu yeyote lakini munaweza kumupa mugeni anayeishi katika miji yenu, akule, au munaweza kumwuzishia mutu wa taifa lingine. Musipike mwana-mbuzi katika maziwa ya mama yake. “Ninyi ni watakatifu na Yawe ni Mungu wenu.