Deuteronomy 14:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ikiwa safari ni ndefu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amechagua mahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali mno na nyumbani, nanyi hamwezi kubeba zaka za mazao yenu ambayo Mwenyezi-Mungu amewajalia kupata, basi, fanyeni hivi:
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale Mwenyezi Mungu atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia Bwana, Mungu wako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ikiwa safari ni ndefu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amechagua mahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali mno na nyumbani, nanyi hamwezi kubeba zaka za mazao yenu ambayo Mwenyezi-Mungu amewajalia kupata, basi, fanyeni hivi:
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na BWANA Mungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale BWANA atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini ikiwa mahali pale ni mbali sana nanyi mmebarikiwa na bwana Mwenyezi Mungu wenu na hamwezi kubeba zaka yenu (kwa sababu mahali pale bwana atakapopachagua kuliweka Jina lake ni mbali sana),
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ikiwa safari ni ndefu kwa kuwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amechagua mahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali mno na nyumbani, nanyi hamwezi kubeba zaka za mazao yenu ambayo Mwenyezi-Mungu amewajalia kupata, basi, fanyeni hivi:
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama safari ya kutoka kwako kwenda huko itakuwa ndefu zaidi, usiweze kuyapeleka hayo matoleo, kwa kuwa ni mbali zaidi kutoka kwako kwenda mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, basi, hapo Bwana Mungu wako atakapokubariki,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na njia ikiwa ndefu mno nawe, usiweze kuzichukua kwa kuwa mahali ni mbali nawe mno atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake, hapo atakapokubarikia BWANA, Mungu wako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ikiwa safari ni ndefu kwa sababu Yawe, Mungu wenu, amechagua pahali pa kuweka jina lake ambapo ni mbali sana na nyumba, nanyi hamuwezi kubeba sehemu ya kumi za mazao yenu ambayo Yawe amewajalia kupata, basi, mufanye hivi: