Deuteronomy 14:26 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
mzitumie hizo fedha kwa chochote kile mtakachopenda — nyama ya ng'ombe, nyama ya kondoo, divai au kinywaji kikali; mtavila na kufurahi hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, pamoja na jamaa zenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ng’ombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na watu wa nyumbani mwenu mtaila mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, na kufurahi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za Bwana, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
mzitumie hizo fedha kwa chochote kile mtakachopenda — nyama ya ng'ombe, nyama ya kondoo, divai au kinywaji kikali; mtavila na kufurahi hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, pamoja na jamaa zenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tumieni hiyo fedha kununua cho chote ukitakacho: ng'ombe, kondoo, divai au kinywaji cho chote chenye chachu au cho chote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele za BWANA Mungu wenu na kufurahi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tumieni hiyo fedha kununua chochote ukitakacho: ng’ombe, kondoo, divai au kinywaji chochote chenye chachu au chochote mnachotaka. Kisha ninyi na wa nyumbani mwenu mtaila mbele za bwana Mwenyezi Mungu wenu na kufurahi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na zile fedha zitumie kwa chochote itakachotamani roho yako, ng'ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako chochote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
mzitumie hizo fedha kwa chochote kile mtakachopenda – nyama ya ng'ombe, nyama ya kondoo, divai au kinywaji kikali; mtavila na kufurahi hapo mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, pamoja na jamaa zenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, utakapoweza kujipatia kwa hizo fedha yote, roho yako itakayotunukia, ng'ombe na mbuzi na kondoo na mvinyo na vileo nayo mengine yote, roho yako itakayoyapenda, ujipatie, kisha utakula hapo mbele ya Bwana Mungu wako, mfurahiwe pamoja wewe nao waliomo nyumbani mwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na zile fedha zitumie kwa cho chote itakachotamani roho yako, ng’ombe, au kondoo, au divai, au kileo, au roho yako itakacho kwako cho chote; nawe utakula huko mbele za BWANA, Mungu wako; tena furahi, wewe na nyumba yako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
muzitumie hizo feza kwa kitu chochote mutakachopenda - nyama ya ngombe, nyama ya kondoo, divai au kinywaji kikali. Mutavikula na kufurahi hapo mbele ya Yawe, Mungu wenu, pamoja na jamaa zenu.