Deuteronomy 14:29 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hiyo itakuwa kwa ajili ya Walawi, kwa kuwa hawana fungu wala urithi wao kati yenu, nao wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu, watakuja kula na kushiba. Fanyeni hivi naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, awabariki katika kazi zenu zote mfanyazo kwa mikono yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba Bwana, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hiyo itakuwa kwa ajili ya Walawi, kwa kuwa hawana fungu wala urithi wao kati yenu, nao wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu, watakuja kula na kushiba. Fanyeni hivi naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, awabariki katika kazi zenu zote mfanyazo kwa mikono yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili BWANA Mungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ili Walawi (ambao hawana mashamba wala urithi wao wenyewe) na wageni, yatima na wajane wanaoishi kwenye miji yenu wapate kuja kula na kushiba, ili bwana Mwenyezi Mungu wenu apate kuwabariki ninyi katika kazi zote za mikono yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hiyo itakuwa kwa ajili ya Walawi, kwa kuwa hawana fungu wala urithi wao kati yenu, nao wageni, yatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu, watakuja kula na kushiba. Fanyeni hivi naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, awabariki katika kazi zenu zote mfanyazo kwa mikono yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha Walawi, kwa kuwa kwako hawana fungu lao la nchi lililo lao wenyewe, na waje pamoja na wageni, nao wliofiwa na wazazi, nao wajane waliomo malangoni mwako, na waje, wale, washibe! Hivyo ndivyo, Bwana Mungu wako atakavyokubarikia kazi zote za mikono yako, utakazozifanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na Mlawi kwa kuwa hana fungu wala urithi pamoja nawe, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio ndani ya malango yako, na waje wale na kushiba; ili kwamba BWANA, Mungu wako, akubarikie katika kazi yote ya mkono wako uifanyayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hiyo itakuwa kwa ajili ya Walawi, kwa sababu hawana fungu wala urizi wao kati yenu, nao wageni, wayatima na wajane ambao wanaishi katika miji yenu, watakuja kula na kushiba. Mufanye hivi naye Yawe, Mungu wenu, atawabariki katika kazi zenu zote munazofanya kwa mikono yenu.