Deuteronomy 14:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini msile mnyama yeyote ambaye kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili na hacheui; msile ngamia, sungura na pelele, ingawa hucheua lakini kwato zao hazikugawanyika sehemu mbili; hao ni najisi kwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini msile mnyama yeyote ambaye kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili na hacheui; msile ngamia, sungura na pelele, ingawa hucheua lakini kwato zao hazikugawanyika sehemu mbili; hao ni najisi kwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo, miongoni mwa wale wanaocheua au wale walio na kwato zilizogawanyika kamwe msile ngamia, sungura na pelele. Iwapo wanacheua, lakini hawana kwato zilizogawanyika; ni najisi kwenu kwa taratibu za kiibada.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini msile mnyama yeyote ambaye kwato zake hazikugawanyika sehemu mbili na hacheui; msile ngamia, sungura na pelele, ingawa hucheua lakini kwato zao hazikugawanyika sehemu mbili; hao ni najisi kwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini nao hao msiwale miongoni mwao wanaocheua namo miongoni mwao walio wenye kwato zilizopasuka na kutengeka: ngamia na sungura na pelele. Kweli wanacheua, lakini hawapasui kwato, kwa hiyo ni mwiko kwenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang’a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini musikule nyama yeyote ambaye kwato zake hazigawanyiki sehemu mbili na hacheui. Musikule ngamia, sungura na pelele, ingawa wanacheua lakini kwato zao hazigawanyiki sehemu mbili; hao ni wachafu kwenu.