Deuteronomy 15:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mpe kwa ukarimu kile ambacho Mwenyezi-Mungu amekubariki: Kondoo, nafaka na divai.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mpe kwa hiari kutoka kundi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka, na kutoka shinikizo lako la kukamulia zabibu. Mpe kama vile Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alivyokubariki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mpe kwa ukarimu kile ambacho Mwenyezi-Mungu amekubariki: kondoo, nafaka na divai.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mpe kwa uhuru kutoka katika zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka katika sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka katika mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyo BWANA Mungu wako alivyokubariki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mpe kwa uhuru kutoka zizi lako la kondoo na mbuzi, kutoka sakafu yako ya kupuria nafaka na kutoka mashinikizo yako ya kukamulia divai. Mpe kama vile ambavyo bwana Mwenyezi Mungu wako alivyokubariki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mpe kwa ukarimu kile ambacho Mwenyezi-Mungu amekubariki: Kondoo, nafaka na divai.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ila umgawie mali kwenda nazo, ukitoa mbuzi na kondoo na mapato ya purio lako, nayo ya kamulio lako. Kwa hivyo, Bwana Mungu wako alivyokubariki, umgawie naye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
umwangalie kwa wema katika kundi lako, na sakafu yako ya nafaka, na kinu chako cha divai; mpe kama alivyokubarikia BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Umupe kwa moyo safi kile ambacho Yawe amekubariki nacho: kondoo, ngano na divai.