Deuteronomy 15:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
basi, utachukua shazia na kutoboa sikio lake mpaka hiyo shazia iingie mlangoni naye atakuwa mtumwa wako milele. Kadhalika mtendee vivyo hivyo mtumwa wako wa kike.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
ndipo utachukua chuma kidogo utoboe sikio lake hadi hicho chuma kiingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mjakazi wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
ndipo utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi chako naye mfanye vivyo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
basi, utachukua shazia na kutoboa sikio lake mpaka hiyo shazia iingie mlangoni naye atakuwa mtumwa wako milele. Kadhalika mtendee vivyo hivyo mtumwa wako wa kike.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
ndipo utachukua chuma ndogo utoboe sikio lake mpaka hiyo chuma iingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mtumishi wa kike.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
ndipo utachukua chuma kidogo utoboe sikio lake mpaka hicho chuma kiingie kwenye ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako wa maisha. Ufanye vivyo hivyo kwa mtumishi wa kike.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
ndipo utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi wako naye mfanye vivyo hivyo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
basi, utachukua shazia na kutoboa sikio lake mpaka hiyo shazia iingie mlangoni naye atakuwa mtumwa wako milele. Kadhalika mtendee vivyo hivyo mtumwa wako wa kike.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
basi, uchukue shazia, ulitoboe sikio lake nalo, kisha umpigilie hivyo mlangoni; ndipo, atakapokuwa mtumwa wako kale na kale. Hata kijakazi utamfanyizia vivyo hivyo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
ndipo utwae uma, uupenyeze katika sikio lake uingie katika ubao wa mlango, naye atakuwa mtumishi wako milele. Na kijakazi chako naye mfanye vivyo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
basi, utatwaa chuma na kutoboa sikio lake mpaka chuma hicho kiingie ndani ya mulango naye atakuwa mutumwa wako milele. Utamutendea mujakazi wako namna hiyohiyo.