Deuteronomy 15:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wala usione ugumu utakapomwacha huru mtumwa wako, maana, amekutumikia kwa muda wa miaka sita kwa nusu ya ujira wa mtumishi wa kuajiri. Fanya hivyo, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako atakubariki kwa kila utakalofanya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. Naye Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atakubariki kwa kila kitu utakachofanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na Bwana, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wala usione ugumu utakapomwacha huru mtumwa wako, maana, amekutumikia kwa muda wa miaka sita kwa nusu ya ujira wa mtumishi wa kuajiri. Fanya hivyo, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako atakubariki kwa kila utakalofanya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. Naye BWANA Mungu wenu atakubarikia kwa kila kitu utakachofanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Usifikiri kuwa kuna ugumu kumwacha mtumishi wako huru, kwa sababu utumishi wake kwako kwa miaka hii sita umekuwa wa thamani mara mbili ya ujira wa mtumishi wa kuajiriwa. Naye bwana Mwenyezi Mungu wenu atakubarikia kwa kila kitu utakachofanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na BWANA, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wala usione ugumu utakapomwacha huru mtumwa wako, maana, amekutumikia kwa muda wa miaka sita kwa nusu ya ujira wa mtumishi wa kuajiri. Fanya hivyo, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako atakubariki kwa kila utakalofanya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Usiyawazie kuwa magumu kumwacha, aondoke kwako kuwa mwungwana tena, kwani atakuwa amekutumikia miaka sita na kufanya kazi za watu wawili wa mshahara, naye Bwana Mungu wako atakubarikia yote, utakayoyafanya.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala usione ugumu, utakapomwacha huru kuondoka kwako; kwani amekutumikia miaka sita kwa ujira mara mbili wa mwajiriwa; na BWANA, Mungu wako, atakubarikia kwa yote utakayofanya.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wala usione ugumu utakapomwacha huru mutumwa wako, maana, amekutumikia kwa muda wa miaka sita kwa nusu ya mushahara wa mutumishi wa kulipwa. Fanya hivyo, naye Yawe, Mungu wako, atakubariki kwa kila utakalofanya.