Deuteronomy 15:19 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtolee Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa kundi lako la ng'ombe na kondoo. Usiwafanyize kazi ng'ombe hao na kondoo hao usiwakate manyoya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wekeni wakfu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya ng’ombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wazaliwa wa kwanza waume wote wazaliwao katika kundi lako la ng'ombe na la kondoo, uwatakase kwa Bwana, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtolee Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa kundi lako la ng'ombe na kondoo. Usiwafanyize kazi ng'ombe hao na kondoo hao usiwakate manyoya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wekeni wakfu kwa BWANA Mungu wenu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya n'gombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wekeni wakfu kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu kila mzaliwa wa kwanza wa kiume wa makundi yenu ya ng’ombe na ya mbuzi na kondoo. Maksai walio wazaliwa wa kwanza msiwafanyize kazi, wala msinyoe manyoya ya wazaliwa wa kwanza wa kondoo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wazaliwa wa kwanza wa kiume wote wazaliwao katika kundi lako la ng'ombe na la kondoo, uwatakase kwa BWANA, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtolee Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, wazaliwa wote wa kwanza wa kiume wa kundi lako la ng'ombe na kondoo. Usiwafanyize kazi ng'ombe hao na kondoo hao usiwakate manyoya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wana wote wa kwanza watakaozaliwa, wao wa ng'ombe wako na wa mbuzi na wa kondoo wako, kama ni wa kiume, sharti uwatakase kuwa wake Bwana Mungu wako, usimtumie kazini mwana wa kwanza wa ng'ombe wako, wala usimkate manyoya mwana wa kwanza wa kondoo wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wazaliwa wa kwanza waume wote wazaliwao katika kundi lako la ng’ombe na la kondoo, uwatakase kwa BWANA, Mungu wako; usifanye kazi kwa mzaliwa wa kwanza wa ng’ombe wako, wala usimkate manyoya mzaliwa wa kwanza wa kundi lako la kondoo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Umutolee Yawe, Mungu wako, wazaliwa wote wa kwanza dume wa kundi lako la ngombe na kondoo. Usiwafanyizishe ngombe hao kazi na kondoo hao usiwakate manyoya.