Deuteronomy 15:21 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini mnyama huyo akiwa na dosari yoyote, yaani akiwa kilema au kipofu, au ana kasoro yoyote kubwa, usimtoe kuwa sadaka kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini akiwa na kilema, akichechea, au akiwa kipofu, au mwenye kilema kibaya cho chote, usimsongezee Bwana, Mungu wako, sadaka.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini mnyama huyo akiwa na dosari yoyote, yaani akiwa kilema au kipofu, au ana kasoro yoyote kubwa, usimtoe kuwa sadaka kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwa BWANA Mungu wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama mnyama ana dosari, akiwa ni kilema au kipofu au kama ana kilema kibaya, kamwe usimtoe dhabihu kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini akiwa na kilema, akichechemea, au akiwa kipofu, au mwenye kilema kibaya chochote, usimsongezee BWANA, Mungu wako, sadaka.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini mnyama huyo akiwa na dosari yoyote, yaani akiwa kilema au kipofu, au ana kasoro yoyote kubwa, usimtoe kuwa sadaka kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini akiwa mwenye kilema, kama ni kiwete au kipofu au mwenye kilema kibaya cho chote, usimchinjie Bwana Mungu wako,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini akiwa na kilema, akichechea, au akiwa kipofu, au mwenye kilema kibaya cho chote, usimsongezee BWANA, Mungu wako, sadaka.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini nyama huyo akiwa na kilema chochote, ni kusema kiwete au kipofu, au ana kilema chochote kikubwa, usimutoe kuwa sadaka kwa Yawe, Mungu wako.