Deuteronomy 15:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki kama vile alivyowaahidi. Nanyi mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa. Kadhalika mtatawala mataifa mengi, lakini mataifa hayo hayatawatawala nyinyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwani Bwana, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki kama vile alivyowaahidi. Nanyi mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa. Kadhalika mtatawala mataifa mengi, lakini mataifa hayo hayatawatawala nyinyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa BWANA Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa ye yote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu atawabariki kama alivyoahidi, nanyi mtawakopesha mataifa mengi lakini hamtakopa kwa yeyote. Mtatawala mataifa mengi lakini hakuna taifa litakalowatawala ninyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwani BWANA, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atawabariki kama vile alivyowaahidi. Nanyi mtayakopesha mataifa mengi, lakini nyinyi hamtakopa. Kadhalika mtatawala mataifa mengi, lakini mataifa hayo hayatawatawala nyinyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana Mungu wako atakubariki, kama alivyokuambia. Kwa hiyo utaweza kukopesha mataifa mengi, lakini mwenyewe hutakopa; hivyo utatawala mataifa mengi, lakini wewe hawatakutawala.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwani BWANA, Mungu wako, atakubarikia, kama alivyokuahidi; nawe utakopesha mataifa mengi, lakini hutakopa; tena utayatawala mataifa mengi, usitawaliwe na wao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe, Mungu wenu, atawabariki kama vile alivyowaahidi. Nanyi mutayakopesha mataifa mengi, lakini ninyi hamutakopa. Vilevile mutatawala mataifa mengi, lakini mataifa hayo hayatawatawala ninyi.