Deuteronomy 15:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kukiwa na maskini wa jamaa yenu katika miji ya nchi ambayo Mwenyezi-Mungu atawapa, msiwe wachoyo na wagumu kwake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa hiyo nchi ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo Bwana, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kukiwa na maskini wa jamaa yenu katika miji ya nchi ambayo Mwenyezi-Mungu atawapa, msiwe wachoyo na wagumu kwake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wo wote wa hiyo nchi ambayo BWANA Mungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa kuna mtu maskini miongoni mwa ndugu zenu, katika mji wowote wa hiyo nchi ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu anawapa, msiwe na moyo mgumu wala usimfumbie mkono ndugu yako aliye maskini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kukiwa na maskini wa jamaa yenu katika miji ya nchi ambayo Mwenyezi-Mungu atawapa, msiwe wachoyo na wagumu kwake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakapokuwa, ndugu yako mmoja aliopo malangoni pako pawapo pote katika nchi yako, Bwana Mungu wako atakayokupa, akose mali, usiushupaze moyo wako, wala usiufunge mkono wako ukimnyima ndugu yako anayetaka kukukopa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama akiwapo mtu maskini pamoja nawe, nduguzo mmojawapo, ndani ya malango yako mojawapo, katika nchi yako akupayo BWANA, Mungu wako, usifanye moyo wako kuwa mgumu, wala usimfumbie mkono wako nduguyo maskini;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kukiwa masikini wa jamaa yenu katika miji ya inchi ambayo Yawe atawapa, musikuwe wachoyo na wagumu kwake.