Deuteronomy 16:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Adhimisheni mwezi wa Abibu na kufanya Pasaka kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Maana katika mwezi huo wa Abibu, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliwatoa Misri wakati wa usiku.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka Bwana, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku Bwana; Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Adhimisheni mwezi wa Abibu na kufanya Pasaka kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Maana katika mwezi huo wa Abibu, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliwatoa Misri wakati wa usiku.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya BWANA Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shikeni mwezi wa Abibu, na kuiadhimisha Pasaka ya bwana Mwenyezi Mungu wenu, kwa sababu katika mwezi wa Abibu, Mungu aliwatoa Misri usiku.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie Pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Adhimisheni mwezi wa Abibu na kufanya Pasaka kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu. Maana katika mwezi huo wa Abibu, Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliwatoa Misri wakati wa usiku.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Uangalie mwezi wa Abibu, ule sikukuu ya Pasaka ya Bwana Mungu wako! Kwani ulikuwa mwezi wa Abibu, Bwana Mungu wako alipokutoa huko Misri na usiku.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utunze mwezi wa Abibu, ukamfanyie pasaka BWANA, Mungu wako, kwa kuwa ilikuwa ni mwezi wa Abibu alipokutoa Misri usiku BWANA; Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mushike mwezi wa Abibu na kufanya Pasaka kwa heshima ya Yawe, Mungu wenu. Maana katika mwezi huo wa Abibu, Yawe, Mungu wenu aliwatoa Misri wakati wa usiku.