Deuteronomy 16:10 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Halafu mtaadhimisha sikukuu ya majuma kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa kutoa sadaka ya hiari, mtakayotoa kadiri awabarikiavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe sikukuu ya majuma umfanyie Bwana, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikiavyo Bwana, Mungu wako;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Halafu mtaadhimisha sikukuu ya majuma kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa kutoa sadaka ya hiari, mtakayotoa kadiri awabarikiavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwa BWANA Mungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayo BWANA Mungu wenu amewapa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha msherehekee Sikukuu ya Majuma kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu kwa kutoa sadaka ya hiari kwa kadiri ya baraka ambayo bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe sikukuu ya majuma umfanyie BWANA, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikivyo BWANA, Mungu wako;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Halafu mtaadhimisha sikukuu ya majuma kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kwa kutoa sadaka ya hiari, mtakayotoa kadiri awabarikiavyo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha na ule sikukuu ya Majuma ya Bwana Mungu wako, mkono wako ukimtolea vipaji kwa furaha ya moyo ya kuvifurahia hivyo, Bwwana Mungu wako alivyokubariki.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe sikukuu ya majuma umfanyie BWANA, Mungu wako, kwa kutoa sadaka ya hiari ya mkono wako, utakayotoa kwa kadiri akubarikiavyo BWANA, Mungu wako;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Halafu mutafanya sikukuu ya majuma kwa heshima ya Yawe, Mungu wenu, kwa kutoa sadaka ya mapenzi kadiri Yawe, Mungu wenu, anavyowabariki.