Deuteronomy 16:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtafurahia mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nyinyi pamoja na wana wenu na binti zenu, watumishi wenu, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi pamoja nanyi. Fanyeni haya katika mahali Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapochagua likae jina lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shangilieni mbele za Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, mahali atakapopachagua kuwa makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane wanaoishi miongoni mwenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawe utafurahi mbele ya Bwana, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua Bwana, Mungu wako, apakalishe jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtafurahia mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nyinyi pamoja na wana wenu na binti zenu, watumishi wenu, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi pamoja nanyi. Fanyeni haya katika mahali Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapochagua likae jina lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shangilieni mbele za BWANA Mungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shangilieni mbele za bwana Mwenyezi Mungu wenu mahali atakapopachagua kama makao ya Jina lake, ninyi, wana wenu na binti zenu, watumishi wenu wa kiume na wa kike, Walawi walio katika miji yenu, na wageni, yatima na wajane waishio miongoni mwenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nawe utafurahi mbele za BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtafurahia mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, nyinyi pamoja na wana wenu na binti zenu, watumishi wenu, Walawi, wageni, yatima na wajane ambao wanaishi pamoja nanyi. Fanyeni haya katika mahali Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, atakapochagua likae jina lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, mtakapofurahi mbele ya Bwana mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake, wewe na mwanao wa kiume na wa kike na mtumishi wako wa kiume na wa kike, naye Mlawi aliopo malangoni pako, nao wageni, nao waliofiwa na wazazi, nao wajane walioko kwako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawe utafurahi mbele ya BWANA, Mungu wako, wewe na mwana wako na binti yako, na mtumwa wako na mjakazi wako, na Mlawi aliye ndani ya malango yako, na mgeni, na yatima, na mjane aliyefiliwa na mumewe, walio katikati yako, katika mahali atakapochagua BWANA, Mungu wako, apakalishe jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutafurahia mbele ya Yawe, Mungu wenu, ninyi pamoja na wana wenu na wabinti zenu, watumishi wenu, Walawi, wageni, wayatima na wajane ambao wanaishi pamoja nanyi. Mufanye haya katika pahali Yawe, Mungu wenu, atakapochagua kwa ajili ya jina lake.