Deuteronomy 16:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa siku saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sherehe mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atapachagua; kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shughuli zenu zote nanyi hakika mtafurahi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, katika mahali atakapopachagua Mwenyezi Mungu. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku saba mfanyie sikukuu Bwana, Mungu wako, mahali atakapochagua Bwana; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, atakubarikia katika maongeo yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa siku saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sherehe mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atapachagua; kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shughuli zenu zote nanyi hakika mtafurahi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya BWANA Mungu wenu katika mahali atakapopachagua BWANA. Kwa kuwa BWANA Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa siku saba mtaiadhimisha sikukuu ya bwana Mwenyezi Mungu wenu katika mahali atakapopachagua bwana. Kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu atawabariki katika mavuno yenu na katika kazi zote za mikono yenu na furaha yenu itakamilika.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubariki katika mavuno yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa siku saba mtamfanyia Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sherehe mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atapachagua; kwa sababu Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shughuli zenu zote nanyi hakika mtafurahi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku saba utaila hiyo sikukuu ya Bwana Mungu wako mahali pale, Bwana atakapopachagua. Kwani Bwana Mungu wako atakubarikia mapato yako yote, nazo kazi zote za mikono yako, kwa hiyo utaweza kuwa mwenye furaha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku saba mfanyie sikukuu BWANA, Mungu wako, mahali atakapochagua BWANA; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, atakubarikia katika maongeo yako yote, na katika kazi zote za mikono yako, nawe uwe katika kufurahi kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa siku saba mutamufanyia Yawe, Mungu wenu, karamu pahali ambapo Yawe atachagua; kwa sababu Yawe, Mungu wenu atawabariki kwa mazao yenu yote na katika shuguli zenu zote nanyi hakika mutafurahi.