Deuteronomy 16:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mtatoa sadaka ya Pasaka kutoka mifugo yenu ya kondoo au ng'ombe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atachagua likae jina lake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo, au la ng’ombe, mahali atakapopachagua Mwenyezi Mungu kuwa makao kwa ajili ya Jina lake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nawe umchinjie pasaka Bwana, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua Bwana apakalishe jina lake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mtatoa sadaka ya Pasaka kutoka mifugo yenu ya kondoo au ng'ombe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atachagua likae jina lake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa BWANA Mungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ng'ombe, mahali pale ambapo BWANA atapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtatoa dhabihu ya Pasaka ya mnyama kwa bwana Mwenyezi Mungu wenu kutoka kundi lenu la mbuzi na kondoo au la ng’ombe, mahali pale ambapo bwana atapachagua kama makao kwa ajili ya Jina lake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nawe umchinjie Pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng'ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mtatoa sadaka ya Pasaka kutoka mifugo yenu ya kondoo au ng'ombe kwa heshima ya Mwenyezi-Mungu mahali ambapo Mwenyezi-Mungu atachagua likae jina lake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo umchinjie Bwana Mungu wako kondoo ya Pasaka, ndio ng'ombe na mbuzi na kondoo, mahali pale, Bwana Mungu wako atakapopachagua kuwa pa kulikalishia Jina lake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nawe umchinjie pasaka BWANA, Mungu wako, katika kundi la kondoo na la ng’ombe, mahali atakapochagua BWANA apakalishe jina lake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mutatoa sadaka ya Pasaka kutoka mifugo yenu ya kondoo au ngombe kwa heshima ya Yawe pahali ambapo Yawe atachagua kwa ajili ya jina lake.