Deuteronomy 16:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa muda wa siku saba mtu yeyote katika nchi yenu asiweke chachu nyumbani mwake; na nyama ya yule mnyama aliyechinjwa jioni ya siku ya kwanza isibaki mpaka asubuhi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Chachu isionekane kwenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yoyote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe hadi asubuhi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa muda wa siku saba mtu yeyote katika nchi yenu asiweke chachu nyumbani mwake; na nyama ya yule mnyama aliyechinjwa jioni ya siku ya kwanza isibaki mpaka asubuhi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hamira isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yo yote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Chachu isionekane katika mali zenu katika nchi yenu yote kwa siku saba. Nyama yoyote ya dhabihu mtakayotoa jioni ya siku ya kwanza isibakizwe mpaka asubuhi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale chochote usiku kucha hata asubuhi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa muda wa siku saba mtu yeyote katika nchi yenu asiweke chachu nyumbani mwake; na nyama ya yule mnyama aliyechinjwa jioni ya siku ya kwanza isibaki mpaka asubuhi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku hizo saba isionekane chachu katika mikate yako, wala nyama za yule kondoo, utakayemchinja siku ya kwanza jioni, zisilale usiku huo hata asubuhi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wala isionekane kwako chachu muda wa siku saba katika mipaka yako yote; wala katika hiyo nyama uchinjayo siku ya kwanza jioni, kisilale cho chote usiku kucha hata asubuhi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa muda wa siku saba mutu yeyote katika inchi yenu asiweke chachu ndani ya nyumba yake, na nyama ya yule nyama aliyechinjwa magaribi ya siku ya kwanza isibaki mpaka asubui.