Deuteronomy 17:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Msimtolee Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sadaka ya ng'ombe au kondoo mwenye dosari, wala ubaya wowote, maana hilo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Msimtolee Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, dhabihu ya maksai au kondoo aliye na dosari yoyote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Usimchinjie Bwana, Mungu wako, ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Msimtolee Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sadaka ya ng'ombe au kondoo mwenye dosari, wala ubaya wowote, maana hilo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Msimtolee BWANA Mungu wenu dhabihu ya maksai au kondoo ambaye ana dosari yo yote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Msimtolee bwana Mwenyezi Mungu wenu dhabihu ya maksai au kondoo ambaye ana dosari yoyote au hitilafu ndani yake, kwa kuwa hilo litakuwa chukizo kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Usimchinjie BWANA, Mungu wako, ng'ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lolote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Msimtolee Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, sadaka ya ng'ombe au kondoo mwenye dosari, wala ubaya wowote, maana hilo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana Mungu wako usimchinjie ng'ombe wala kondoo mwenye kilema au kibaya cho chote! Kwani hayo humchukiza Bwana Mungu wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Usimchinjie BWANA, Mungu wako, ng’ombe wala kondoo aliye na kilema, wala neno ovu lo lote; kwa kuwa hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Musitoe sadaka kwa Yawe, Mungu wenu, ngombe au kondoo mwenye kilema; hiyo ni chukizo kwa Yawe, Mungu wenu.