Deuteronomy 17:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mtakapokwisha ingia katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni, mkaimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, ‘Tutaweka mfalme juu yetu, kama mataifa yote yanayotuzunguka;’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utakapoingia katika nchi anayowapa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mtakapokwisha ingia katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni, mkaimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, ‘Tutaweka mfalme juu yetu, kama mataifa yote yanayotuzunguka;’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati utakapoingia katika nchi anayowapa BWANA Mungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati utakapoingia katika nchi anayowapa bwana Mwenyezi Mungu wenu kuimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, “Na tumweke mfalme juu yetu kama mataifa yanayotuzunguka,”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kandokando yangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mtakapokwisha ingia katika nchi ambayo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, anawapeni, mkaimiliki na kukaa humo, nanyi mkasema, ‘Tutaweka mfalme juu yetu, kama mataifa yote yanayotuzunguka;’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utakapoingia katika nchi hiyo, Bwana Mungu wako atakayokupa, uichukue, iwe yako, ukae huko, ndipo, utakaposema: Na nijiwekee mfalme, kama mataifa yote yanayokaa na kunizunguka pande zote yalivyo na wafalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utakapokwisha kuingia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako ukaimiliki, na kukaa humo; nawe utakaposema, Nitaweka mfalme juu yangu mfano wa mataifa yote yaliyo kando-kando yangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mutakapokwisha kuingia katika inchi ambayo Yawe, Mungu wenu, anawapa, mukirizi na kukaa humo, nanyi mukisema kwamba mutaweka mufalme juu yenu, kama vile mataifa yote yanayowazunguka,