Deuteronomy 18:16 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Hicho ndicho mlichomwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kule Horebu, siku ile mlipokusanyika na kusema, ‘Tusisikie tena sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala tusiuone tena moto huu mkubwa, tusije tukafa!’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kama vile ulivyotaka kwa Bwana, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya Bwana, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Hicho ndicho mlichomwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kule Horebu, siku ile mlipokusanyika na kusema, ‘Tusisikie tena sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala tusiuone tena moto huu mkubwa, tusije tukafa!’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba BWANA Mungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya BWANA Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa kuwa hivi ndivyo mlivyomwomba bwana Mwenyezi Mungu wenu kule Horebu siku ile ya kusanyiko, wakati mliposema, “Na tusiisikie sauti ya bwana Mwenyezi Mungu wetu, wala kuuona moto huu mkubwa tena, ama sivyo tutakufa.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kama vile ulivyotaka kwa BWANA, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya BWANA, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Hicho ndicho mlichomwomba Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, kule Horebu, siku ile mlipokusanyika na kusema, ‘Tusisikie tena sauti ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wetu, wala tusiuone tena moto huu mkubwa, tusije tukafa!’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni kwa ajili yao yote, uliyomwomba Bwana Mungu wako kule Horebu siku hiyo ya mkutano kwamba: Nisiendelee kuisikia sauti ya Bwana Mungu wangu na kuuona huu moto mkubwa, nisife.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kama vile ulivyotaka kwa BWANA, Mungu wako, huko Horebu, siku ya kusanyiko, ukisema, Nisisikie tena sauti ya BWANA, Mungu wangu, wala nisiuone tena moto huu mkubwa, nisije nikafa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hicho ndicho mulichomwomba Yawe, Mungu wenu, kule Horebu, siku ile mulipokusanyika na kusema: ‘Tusisikie tena sauti ya Yawe, Mungu wetu, wala tusiuone tena moto huu mukubwa, kusudi tusikufe!’