Deuteronomy 18:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama nabii akisema kitu ati kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kitu hicho hakifanyiki au hakiwi kweli, jambo hilo hakulisema Mwenyezi-Mungu; nabii amelisema kwa ufidhuli, nanyi msitishwe na jambo hilo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la Mwenyezi Mungu hakikutendeka au kutimia, huo ni ujumbe ambao Mwenyezi Mungu hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Atakaponena nabii kwa jina la Bwana, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena Bwana; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama nabii akisema kitu ati kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kitu hicho hakifanyiki au hakiwi kweli, jambo hilo hakulisema Mwenyezi-Mungu; nabii amelisema kwa ufidhuli, nanyi msitishwe na jambo hilo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la BWANA hakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambao BWANA hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa kile nabii anachotangaza kwa jina la bwana hakikutokea au kutimia, huo ni ujumbe ambao bwana hakusema. Nabii huyo amesema kwa ujuaji. Msimwogope huyo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama nabii akisema kitu ati kwa jina la Mwenyezi-Mungu, na kitu hicho hakifanyiki au hakiwi kweli, jambo hilo hakulisema Mwenyezi-Mungu; nabii amelisema kwa ufidhuli, nanyi msitishwe na jambo hilo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ni hivi: mfumbuaji akisema neno kwa Jina la Bwana, lakini hilo neno haliji, wala halitimii, basi, hilo ndilo neno, Bwana asilolisema, yule mfumbuaji amelisema kwa kujikuza tu, kwa hiyo usimwogope!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Atakaponena nabii kwa jina la BWANA, lisifuate jambo lile wala kutimia, hilo ndilo neno asilolinena BWANA; kwa kujikinai amelinena huyo nabii, usimwogope
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama nabii akisema kitu aseme ni kwa jina la Yawe, na kitu hicho hakifanyiki au hakiko kweli, jambo hilo Yawe hakulisema; nabii amelisema kwa kiburi, nanyi musitishwe na jambo hilo.