Deuteronomy 19:15 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ushahidi wa mtu mmoja hautoshi kumhukumu mtu juu ya kosa lolote la jinai au uovu kuhusu kosa lolote alilofanya. Ni ushahidi wa watu wawili au watatu tu ndio utakaothaminiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Shahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lolote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lolote lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wo wote, wala kwa dhambi yo yote, katika makosa akosayo yo yote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ushahidi wa mtu mmoja hautoshi kumhukumu mtu juu ya kosa lolote la jinai au uovu kuhusu kosa lolote alilofanya. Ni ushahidi wa watu wawili au watatu tu ndio utakaothaminiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Shahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lo lote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Shahidi mmoja hatoshi kumtia hatiani mtu kwa uhalifu au kosa lolote ambalo anaweza kuwa amelitenda. Lazima shauri lolote lithibitishwe kwa ushuhuda wa mashahidi wawili au watatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wowote, wala kwa dhambi yoyote, katika makosa akosayo yoyote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ushahidi wa mtu mmoja hautoshi kumhukumu mtu juu ya kosa lolote la jinai au uovu kuhusu kosa lolote alilofanya. Ni ushahidi wa watu wawili au watatu tu ndio utakaothaminiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu mmoja asimwondokee mwingine katika shauri la manza zo zote, wala la ukosaji wo wote uliomkosesha mtu kosa lo lote, watu wanalolikosa, ila shauri litawezekana tu kwa ushahidi wa watu wawili au watatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Shahidi mmoja asimwinukie mtu awaye yote kumshuhudia kwa uovu wo wote, wala kwa dhambi yo yote, katika makosa akosayo yo yote; jambo na lithibitishwe kwa vinywa vya mashahidi wawili, au watatu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ushuhuda wa mutu mumoja hautoshi kwa kuhukumu mutu juu ya kosa lolote au uovu juu ya kosa lolote alilofanya. Ni ushuhuda wa watu wawili au watatu tu ndio utakaohakishwa.