Deuteronomy 2:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kisha, tuligeuka, tukasafiri jangwani kwa kupitia njia ya Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi-Mungu alivyoniambia; tulitangatanga karibu na mlima Seiri kwa muda mrefu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha tukageuka nyuma na kusafiri kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi Mungu alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea kuzunguka nchi ya vilima ya Seiri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ndipo tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia Bwana; tukawa kuizunguka milima ya Seiri siku nyingi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kisha, tuligeuka, tukasafiri jangwani kwa kupitia njia ya Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi-Mungu alivyoniambia; tulitangatanga karibu na mlima Seiri kwa muda mrefu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha tukageuka nyuma na kusafiri kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kama BWANA alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea kuzunguka vilima katika nchi ya Seiri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha tukageuka nyuma na kusafiri kuelekea jangwani kwa njia inayoelekea Bahari ya Shamu, kama bwana alivyonielekeza. Kwa muda mrefu tulitembea kuzunguka vilima katika nchi ya Seiri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ndipo tukageuka, tukashika maisha ya jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia BWANA; tukaizunguka milima ya Seiri siku nyingi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kisha, tuligeuka, tukasafiri jangwani kwa kupitia njia ya Bahari ya Shamu, kama Mwenyezi-Mungu alivyoniambia; tulitangatanga karibu na mlima Seiri kwa muda mrefu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha tukageuka na kuondoka huko, turudi nyikani na kushika nja ya kwenda kwenye Bahari Nyekundu, kama Bwana alivyoniambia, tukazunguka siku nyingi kwenye mlima wa Seiri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ndipo tukageuka, tukashika safari yetu kwenda jangwani kwa njia ya Bahari ya Shamu, kama alivyoniambia BWANA; tukawa kuizunguka milima ya Seiri siku nyingi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kisha, tukageuka, tukasafiri katika jangwa kwa kupitia njia ya bahari Nyekundu, kama vile Yawe alivyoniambia. Tukatangatanga karibu na mulima Seiri kwa muda murefu.