Deuteronomy 2:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wahori pia waliishi huko Seiri hapo awali, lakini wazawa wa Esau waliwafukuza na kuwaangamiza, kisha wao wenyewe wakakaa katika eneo hilo badala yao. Waisraeli walifanya vivyo hivyo katika nchi ile ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa iwe mali yao).
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wahori waliishi Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafukuza. Waliwaangamiza Wahori na kukaa mahali pao, kama Waisraeli walivyofanya katika nchi ambayo Mwenyezi Mungu aliwapa kama milki yao.)
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Wahori nao walikuwa wakikaa Seiri hapo kale, lakini wana wa Esau waliwafuata; wakawaangamiza mbele yao, wakakaa badala yao; kama alivyofanya Israeli nchi ya milki yake aliyopewa na Bwana.)
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wahori pia waliishi huko Seiri hapo awali, lakini wazawa wa Esau waliwafukuza na kuwaangamiza, kisha wao wenyewe wakakaa katika eneo hilo badala yao. Waisraeli walifanya vivyo hivyo katika nchi ile ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa iwe mali yao).
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wahori waliishi Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafukuza. Waliwaangamiza Wahori na kukaa mahali pao, kama Waisraeli walivyofanya katika nchi ambayo BWANA aliwapa kama milki yao.)
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wahori waliishi Seiri, lakini wazao wa Esau waliwafukuza. Waliwaangamiza Wahori na kukaa mahali pao, kama Waisraeli walivyofanya katika nchi ambayo bwana aliwapa kama milki yao.)
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na Wahori nao walikuwa wakikaa Seiri hapo kale, lakini wazawa wa Esau waliwafuata; wakawaangamiza mbele yao, wakakaa badala yao; kama alivyofanya Israeli nchi ya milki yake aliyopewa na BWANA.)
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wahori pia waliishi huko Seiri hapo awali, lakini wazawa wa Esau waliwafukuza na kuwaangamiza, kisha wao wenyewe wakakaa katika eneo hilo badala yao. Waisraeli walifanya vivyo hivyo katika nchi ile ambayo Mwenyezi-Mungu aliwapa iwe mali yao).
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Huko Seiri kale walikaa Wahori; ndio, wana wa Esau waliowafukuza na kuwaangamiza mbele yao, kisha wakakaa mahali pao, kama Waisiraeli walivyofanya katika nchi, waliyoichukua, iwe yao, Bwana aliyowapa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na Wahori nao walikuwa wakikaa Seiri hapo kale, lakini wana wa Esau waliwafuata; wakawaangamiza mbele yao, wakakaa badala yao; kama alivyofanya Israeli nchi ya milki yake aliyopewa na BWANA.)
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wahori vilevile waliishi huko Seiri zamani, lakini wazao wa Esau wakawafukuza na kuwaangamiza, kisha wao wenyewe wakakaa katika eneo hilo pahali pao. Waisraeli wakafanya vile vile katika inchi ile ambayo Yawe aliwapa ikuwe mali yao.)