Deuteronomy 2:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Miaka thelathini na nane ilikuwa imepita tangu kuondoka Kadesh-barnea mpaka kuvuka kijito cha Zeredi. Wakati huo, kizazi chote cha wale watu wa umri wa kwenda vitani kilikuwa kimetoweka kulingana na jinsi Mwenyezi-Mungu alivyowaapia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Miaka thelathini na nane ilipita tangu wakati tuliondoka Kadesh-Barnea hadi tulipovuka Bonde la Zeredi. Kwa wakati huo kile kizazi chote cha wanaume walioweza kwenda vitani kilikuwa kimekufa, kama Mwenyezi Mungu alivyokuwa amewaapia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na siku tulizokuwa tukienda kutoka Kadesh-barnea hata tulipovuka kijito cha Zeredi, zilikuwa ni miaka thelathini na minane; maana, hata walipokwisha kuangamizwa watu wa vita kutoka kati ya marago, kizazi chao chote, kama walivyoapiwa na Bwana.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Miaka thelathini na nane ilikuwa imepita tangu kuondoka Kadesh-barnea mpaka kuvuka kijito cha Zeredi. Wakati huo, kizazi chote cha wale watu wa umri wa kwenda vitani kilikuwa kimetoweka kulingana na jinsi Mwenyezi-Mungu alivyowaapia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Miaka thelathini na minane ilipita tangu wakati tulipoondoka Kadesh-Barnea mpaka tulipovuka Bonde la Zeredi. Kwa wakati huo kile kizazi chote cha wanaume kuanzia wale wawezao kwenda vitani kilikuwa kimekufa, kama BWANA alivyokuwa amewaapia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Miaka thelathini na minane ilipita tangu wakati tulipoondoka Kadesh-Barnea mpaka tulipovuka Bonde la Zeredi. Kwa wakati huo kile kizazi chote cha wanaume kuanzia wale wawezao kwenda vitani kilikuwa kimekufa, kama bwana alivyokuwa amewaapia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na siku tulizokuwa tukienda kutoka Kadesh-barnea hata tulipovuka kijito cha Zeredi, ilikuwa ni miaka thelathini na minane; maana, hata walipokwisha kuangamizwa watu wa vita kutoka kati ya kambi, kizazi chao chote, kama walivyoapiwa na BWANA.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Miaka thelathini na nane ilikuwa imepita tangu kuondoka Kadesh-barnea mpaka kuvuka kijito cha Zeredi. Wakati huo, kizazi chote cha wale watu wa umri wa kwenda vitani kilikuwa kimetoweka kulingana na jinsi Mwenyezi-Mungu alivyowaapia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nazo siku, tulizosafiri toka Kadesi-Barnea mpaka tulipokivuka kijito cha Zeredi, zilikuwa miaka 38; ndipo, kile kizazi chote cha wapiga vita kilipokuwa kimeishilizwa makambini, kama Bwana alivyowaapia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na siku tulizokuwa tukienda kutoka Kadesh-barnea hata tulipovuka kijito cha Zeredi, zilikuwa ni miaka thelathini na minane; maana, hata walipokwisha kuangamizwa watu wa vita kutoka kati ya marago, kizazi chao chote, kama walivyoapiwa na BWANA.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Miaka makumi tatu na nane ilikuwa imepita tangu kuondoka Kadesi-Barnea mpaka kuvuka kijito Zeredi. Wakati huo, wote wenye umri wa kwenda kwa vita waliotoka Misri walikuwa wamekwisha kufa, kulingana na jinsi Yawe alivyowaapia.