Deuteronomy 2:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu alifanya kama alivyowafanyia wazawa wa Esau, Waedomu, ambao wanaishi katika nchi ya Seiri. Aliwaangamiza Wahori wakati Waedomu walipofika huko, wakainyakua nchi yao na kuishi humo hadi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu alikuwa amefanya vivyo hivyo kwa wazao wa Esau, ambao waliishi Seiri, alipowaangamiza Wahori watoke mbele yao. Waliwafukuza na wao wakaishi mahali pao hadi leo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
kama vile alivyowafanyia wana wa Esau, waliokaa Seiri, alipowaangamiza Wahori mbele yao; wakawafuata, wakakaa badala yao hata hivi leo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu alifanya kama alivyowafanyia wazawa wa Esau, Waedomu, ambao wanaishi katika nchi ya Seiri. Aliwaangamiza Wahori wakati Waedomu walipofika huko, wakainyakua nchi yao na kuishi humo hadi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA alikuwa amefanya vivyo hivyo kwa wazao wa Esau, ambao waliishi Seiri, wakati alipowaangamiza Wahori watoke mbele yao. Waliwafukuza na wao wakaishi mahali pao mpaka leo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana alikuwa amefanya vivyo hivyo kwa wazao wa Esau, ambao waliishi Seiri, wakati alipowaangamiza Wahori watoke mbele yao. Waliwafukuza na wao wakaishi mahali pao mpaka leo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
kama vile alivyowafanyia wana wa Esau, waliokaa Seiri, alipowaangamiza Wahori mbele yao; wakawafuata, wakakaa badala yao hadi hivi leo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu alifanya kama alivyowafanyia wazawa wa Esau, Waedomu, ambao wanaishi katika nchi ya Seiri. Aliwaangamiza Wahori wakati Waedomu walipofika huko, wakainyakua nchi yao na kuishi humo hadi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ni vivyo hivyo, alivyowafanyizia wana wa Esau wanaokaa Seiri, maana mbele yao waliwaangamiza Wahori, wapate kuichukua nchi yao na kukaa huko mahali pao mpaka siku hii ya leo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
kama vile alivyowafanyia wana wa Esau, waliokaa Seiri, alipowaangamiza Wahori mbele yao; wakawafuata, wakakaa badala yao hata hivi leo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe akafanya kama vile alivyowafanyia wazao wa Esau ndio Waedomu, ambao wanaishi katika inchi ya Seiri. Aliwaangamiza Wahori wakati Waedomu walipofika huko, wakanyanganya inchi yao na kuishi humo mpaka leo.