Deuteronomy 2:30 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Lakini Sihoni, mfalme wa Heshboni, hakuturuhusu tupite nchini mwake. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alimfanya awe na kichwa kigumu na mkaidi wa moyo, ili tumshinde na kuchukua nchi yake ambayo tunaimiliki hadi leo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni alikataa kuturuhusu kupita. Kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, alikuwa ameifanya roho yake kuwa ngumu na moyo wake kuwa mkaidi ili amweke kwenye mikono yenu, kama alivyofanya sasa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa Bwana, Mungu wako, alimfanya mgumu roho yake, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate mtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Lakini Sihoni, mfalme wa Heshboni, hakuturuhusu tupite nchini mwake. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alimfanya awe na kichwa kigumu na mkaidi wa moyo, ili tumshinde na kuchukua nchi yake ambayo tunaimiliki hadi leo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni alikataa kuturuhusu kupita. Kwa kuwa BWANA Mungu wako alikuwa ameifanya roho yake kuwa ngumu na moyo wake kuwa mkaidi ili amweke kwenye mikono yenu, kama alivyofanya sasa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni alikataa kuturuhusu kupita. Kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wako alikuwa ameifanya roho yake kuwa ngumu na moyo wake kuwa mkaidi ili amweke kwenye mikono yenu, kama alivyofanya sasa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alifanya roho yake kuwa ngumu, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate kumtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Lakini Sihoni, mfalme wa Heshboni, hakuturuhusu tupite nchini mwake. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, alimfanya awe na kichwa kigumu na mkaidi wa moyo, ili tumshinde na kuchukua nchi yake ambayo tunaimiliki hadi leo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini Sihoni, mfalme wa Hesiboni, hakutaka kutupa ruhusa ya kupita kwake, kwa kuwa Bwana Mungu wako alimpa mawazo magumu rohoni na kuushupaza moyo wake, apate kumtia mikononi mwako, kama inavyoelekea sasa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini Sihoni mfalme wa Heshboni hakutuacha kupitia kwake; kwa kuwa BWANA, Mungu wako, alimfanya mgumu roho yake, akamtia ukaidi moyoni mwake, apate mtia mkononi mwako kama alivyo hivi leo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Lakini Sihoni, mufalme wa Hesiboni, hakuturuhusu tupite katika inchi yake. Yawe, Mungu wenu, akamufanya akuwe na kichwa kigumu na mugumu wa moyo, kusudi tumushinde na kutwaa inchi yake ambayo tunairizi mpaka leo.