Deuteronomy 2:36 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kuanzia Aroeri, mji ulio ukingoni mwa bonde la Arnoni na mji ulio ndani ya bonde hili mpaka Gileadi, hakuna mji wowote uliokuwa imara hata tukashindwa kuuteka. Mwenyezi-Mungu aliitia yote mikononi mwetu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kutoka mji ulio ndani ya bonde, hadi kufika Gileadi, hapakuwa na mji hata mmoja uliokuwa na nguvu kutushinda. Mwenyezi Mungu, Mungu wetu, alitupatia yote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kutushinda; Bwana, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisongelea;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kuanzia Aroeri, mji ulio ukingoni mwa bonde la Arnoni na mji ulio ndani ya bonde hili mpaka Gileadi, hakuna mji wowote uliokuwa imara hata tukashindwa kuuteka. Mwenyezi-Mungu aliitia yote mikononi mwetu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kutoka mji ulio ndani ya bonde, hata mpaka Gileadi, hapakuwa na mji hata mmoja uliokuwa na nguvu kutushinda. BWANA Mungu wetu alitupa yote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka Aroeri kwenye ukingo wa Bonde la Arnoni, kutoka mji ulio ndani ya bonde, hata mpaka Gileadi, hapakuwa na mji hata mmoja uliokuwa na nguvu kutushinda. bwana Mwenyezi Mungu wetu alitupa yote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa na ngome ndefu ya kutushinda; BWANA, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisogelea;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kuanzia Aroeri, mji ulio ukingoni mwa bonde la Arnoni na mji ulio ndani ya bonde hili mpaka Gileadi, hakuna mji wowote uliokuwa imara hata tukashindwa kuuteka. Mwenyezi-Mungu aliitia yote mikononi mwetu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toka Aroeri ulioko ukingoni kwenye kijito cha Arnoni, katika miji iliyoko kule kwenye kijito mpaka Gileadi haukuwako mji wenye boma refu la kutushinda, yote pia Bwana Mungu wetu aliitoa mbele yetu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kutoka Aroeri iliyo katika ukingo wa bonde la Arnoni, na huo mji ulio ndani ya bonde, mpaka kufika Gileadi, hapakuwa na mji uliokuwa mrefu kutushinda; BWANA, Mungu wetu, aliiweka wazi yote mbele yetu; ila nchi ya wana wa Amoni hukuisongelea;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuanzia Aroeri, muji unaokuwa kwenye ukingo wa bonde la Arnoni, na ule muji mwingine unaokuwa ndani ya bonde hili mpaka inchi ya Gileadi, hakuna muji wowote ambao hatukuweza kuushinda. Yawe aliitia miji yote katika mikono yetu.