Deuteronomy 2:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Basi, kumbukeni jinsi Mwenyezi-Mungu Mungu wenu alivyowabariki katika kila jambo mlilofanya. Aliwatunza mlipokuwa mnatangatanga katika jangwa hili kubwa. Amekuwa pamoja nanyi miaka hii yote arubaini na hamkupungukiwa kitu chochote.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewabariki kwa kazi yote ya mikono yenu. Amewalinda katika safari yenu katikati ya jangwa hili kubwa. Kwa miaka hii arobaini Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amekuwa pamoja nanyi, na hamkupungukiwa na kitu chochote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa kuwa Bwana, Mungu wako, amekubarikia katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arobaini hii alikuwa nawe Bwana, Mungu wako; hukukosa kitu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Basi, kumbukeni jinsi Mwenyezi-Mungu Mungu wenu alivyowabariki katika kila jambo mlilofanya. Aliwatunza mlipokuwa mnatangatanga katika jangwa hili kubwa. Amekuwa pamoja nanyi miaka hii yote arubaini na hamkupungukiwa kitu chochote.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mungu wenu amewabariki kwa kazi yote ya mikono yenu. Amewalinda katika safari yenu katikati ya jangwa hili kubwa. Kwa miaka hii arobaini BWANA Mungu wenu amekuwa pamoja nanyi, na hamkupungukiwa na kitu cho chote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenyezi Mungu wenu amewabariki kwa kazi yote ya mikono yenu. Amewalinda katika safari yenu katikati ya jangwa hili kubwa. Kwa miaka hii arobaini bwana Mwenyezi Mungu wenu amekuwa pamoja nanyi, na hamkupungukiwa na kitu chochote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubariki katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arobaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Basi, kumbukeni jinsi Mwenyezi-Mungu Mungu wenu alivyowabariki katika kila jambo mlilofanya. Aliwatunza mlipokuwa mnatangatanga katika jangwa hili kubwa. Amekuwa pamoja nanyi miaka hii yote arubaini na hamkupungukiwa kitu chochote.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani Bwana Mungu wako amekubariki katika mambo yote, uliyoyafanya kwa mkono wako, anazijua safari zako, ulizozifanya katika nyika hii kubwa; hii miaka arobaini Bwana Mungu wako amekuwa pamoja na wewe, usikose cho chote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa kuwa BWANA, Mungu wako, amekubarikia katika kazi yote ya mkono wako; amejua ulivyotembea katika jangwa kubwa hili; miaka arobaini hii alikuwa nawe BWANA, Mungu wako; hukukosa kitu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Basi, mukumbuke jinsi Yawe Mungu wenu alivyowabariki ninyi katika kila jambo mulilofanya. Aliwatunza mulipokuwa munatangatanga katika jangwa hili kubwa. Amekuwa pamoja nanyi miaka hii yote makumi ine na hamukupungukiwa na kitu chochote.