Deuteronomy 20:1 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Mkienda vitani kupigana na adui zenu, mkaona farasi, magari na jeshi kubwa zaidi kuliko lenu msiwaogope. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliyewatoa Misri, atakuwa nanyi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtakapoenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa Bwana Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Mkienda vitani kupigana na adui zenu, mkaona farasi, magari na jeshi kubwa zaidi kuliko lenu msiwaogope. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliyewatoa Misri, atakuwa nanyi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu BWANA Mungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mtakapokwenda vitani kupigana na adui zenu na mkaona farasi na magari ya vita na jeshi kubwa kuliko lenu, msiwaogope, kwa sababu bwana Mwenyezi Mungu wenu aliyewatoa kutoka Misri, atakuwa pamoja nanyi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Mkienda vitani kupigana na adui zenu, mkaona farasi, magari na jeshi kubwa zaidi kuliko lenu msiwaogope. Maana Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu aliyewatoa Misri, atakuwa nanyi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utakapotoka kwenda vitani kupigana na adui zako, ukaona farasi na magari na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope! Kwani Bwana Mungu wako aliyekutoa katika nchi ya Misri kukuleta huku yuko pamoja na wewe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utokapo kwenda vitani kupigana na adui zako, na kuona farasi, na magari, na watu wengi kuliko wewe, usiwaogope; kwa kuwa BWANA Mungu wako, yu pamoja nawe, aliyekukweza kutoka nchi ya Misri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mukienda kwa vita kupigana na waadui zenu, mukiona farasi, magari na jeshi kubwa zaidi kuliko lenu musiwaogope. Maana Yawe, Mungu wenu, aliyewatoa Misri, atakuwa nanyi.