Deuteronomy 20:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
lakini wanawake na watoto, ng'ombe, na vyote vilivyomo mjini, nyara zake zote mwaweza kuchukua mateka kwa ajili yenu wenyewe; mnaweza kufurahia nyara za adui zenu, ambazo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewapa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine chochote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazo Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewapa kutoka kwa adui zenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
lakini wanawake na watoto, ng'ombe, na vyote vilivyomo mjini, nyara zake zote mwaweza kuchukua mateka kwa ajili yenu wenyewe; mnaweza kufurahia nyara za adui zenu, ambazo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewapa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine cho chote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazo BWANA Mungu wenu amewapa kutoka kwa adui zenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa upande wa wanawake, watoto, mifugo na kila kitu kingine chochote ndani ya huo mji, mnaweza kuvichukua kama nyara kwa ajili yenu. Nanyi mnaweza kuzitumia hizo nyara ambazo bwana Mwenyezi Mungu wenu amewapa kutoka kwa adui zenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
lakini wanawake na watoto, ng'ombe, na vyote vilivyomo mjini, nyara zake zote mwaweza kuchukua mateka kwa ajili yenu wenyewe; mnaweza kufurahia nyara za adui zenu, ambazo Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, amewapa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini wanawake na watoto na nyama wa kufuga nayo yote yatakayokuwa humo mjini na ujitwalie yote pia kuwa mateka yako ya humo mjini, nawe utaweza kula mateka ya adui zako, Bwana Mungu wako atakayokupa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
lakini wanawake na watoto, na wanyama wa miji, na vilivyo mjini vyote, navyo ni nyara zake zote, uvitwae viwe mateka kwako; nawe utakula nyara za adui zako alizokupa BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini wanawake na watoto, ngombe, na vyote vinavyokuwa katika muji, vitu vyake vyote munaweza kuvibeba kwa ajili yenu wenyewe. Munaweza kufurahia vitu vya waadui zenu, ambavyo Yawe, Mungu wenu, amewapa.