Deuteronomy 20:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
wasije wakawafundisha desturi zao za kuchukiza ambazo waliifanyia miungu yao, nanyi mkatenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi ya Mwenyezi Mungu, Mungu wenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya Bwana, Mungu wenu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
wasije wakawafundisha desturi zao za kuchukiza ambazo waliifanyia miungu yao, nanyi mkatenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi ya BWANA Mungu wenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
La sivyo, watawafundisha kufuata mambo yote ya machukizo wanayofanya wakiabudu miungu yao, nanyi mtatenda dhambi dhidi ya bwana Mwenyezi Mungu wenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya BWANA, Mungu wenu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
wasije wakawafundisha desturi zao za kuchukiza ambazo waliifanyia miungu yao, nanyi mkatenda dhambi dhidi ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
kusudi wasiwafundishe ninyi kuyafanya hayo matapisho yote, waliyoifanyizia miungu yao, ninyi mkamkosea Bwana Mungu wenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
wasije wakawafunza kufanya mfano wa machukizo yao yote, waliyoifanyia miungu yao; hivyo itakuwa ni makosa juu ya BWANA, Mungu wenu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
kusudi wasiwafundishe desturi zao za kuchukiza ambazo wanafanyia miungu yao, nanyi mutende zambi mbele ya Yawe, Mungu wenu.