Deuteronomy 21:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
na kubadili nguo zake za mateka. Atakaa muda wa mwezi mzima kumwombolezea baba yake na mama yake; kisha waweza kumwoa uwe mume wake, naye awe mke wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapomwendea, uwe mume wake naye atakuwa mke wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
avue na mavazi ya uteka wake akae nyumbani mwako, awakalie matanga babaye na mamaye mwezi mzima, kisha uingie kwake uwe mumewe, naye awe mkeo.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
na kubadili nguo zake za mateka. Atakaa muda wa mwezi mzima kumwombolezea baba yake na mama yake; kisha waweza kumwoa uwe mume wake, naye awe mke wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
avue nguo alizokuwa amevaa alipotekwa. Baada ya kuishi nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake kwa mwezi mzima, ndipo utakapoweza kumwendea na kuwa mume wake naye atakuwa mke wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
avue na mavazi ya uteka wake akae nyumbani mwako, awakalie matanga babaye na mamaye mwezi mzima, kisha uingie kwake uwe mumewe, naye awe mkeo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
na kubadili nguo zake za mateka. Atakaa muda wa mwezi mzima kumwombolezea baba yake na mama yake; kisha waweza kumwoa uwe mume wake, naye awe mke wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
azivue nazo nguo, alizokuwa amezivaa alipotekwa, akae nyumbani mwako na kumwombolezea baba yake na mama yake mwezi mzima, kisha utaingia kwake, uwe mumewe, naye awe mkeo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
avue na mavazi ya uteka wake akae nyumbani mwako, awakalie matanga babaye na mamaye mwezi mzima, kisha uingie kwake uwe mumewe, naye awe mkeo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kubadilisha nguo zake za kitumwa. Atakaa muda wa mwezi muzima kwa kumwomboleza baba yake na mama yake. Kisha mwanaume huyo anaweza kumwoa.