Deuteronomy 21:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nao makuhani wa ukoo wa Lawi sharti wawepo hapo. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliwachagua wamhudumie na kubariki watu kwa jina lake. Wao pia ndio wenye mamlaka kuhusu kila tukio na utumiaji wa nguvu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Makuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwa Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina la Mwenyezi Mungu, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nao makuhani wana wa Lawi wasongee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua Bwana, Mungu wako, wamtumikie, na kubariki katika jina la Bwana na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo, litakuwa kwa kufuata maneno yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nao makuhani wa ukoo wa Lawi sharti wawepo hapo. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliwachagua wamhudumie na kubariki watu kwa jina lake. Wao pia ndio wenye mamlaka kuhusu kila tukio na utumiaji wa nguvu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Makuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwa BWANA Mungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina la BWANA, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Makuhani, hao wana wa Lawi, watasogea mbele, kwa kuwa bwana Mwenyezi Mungu wenu, amewachagua kuhudumu na kutoa baraka katika jina la bwana, na kuamua mashauri yote ya mabishano na mashambulio.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nao makuhani wana wa Lawi wasogee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua BWANA, Mungu wako, wamtumikie, na kubariki katika jina la BWANA na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo, litakuwa kwa kufuata maneno yao;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nao makuhani wa ukoo wa Lawi sharti wawepo hapo. Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu, aliwachagua wamhudumie na kubariki watu kwa jina lake. Wao pia ndio wenye mamlaka kuhusu kila tukio na utumiaji wa nguvu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha watambikaji Walawi na waje huko, kwani Bwana Mungu wako aliwachagua kumtumikia na kubariki katika Jina lake Bwana, magomvi yote na mapigano yote yamalizwe kwa kusema kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nao makuhani wana wa Lawi wasongee karibu, kwa kuwa ndio aliowachagua BWANA, Mungu wako, wamtumikie, na kubariki katika jina la BWANA na kila neno lishindaniwalo, na kila pigo, litakuwa kwa kufuata maneno yao;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nao makuhani wa ukoo wa Lawi sharti wakuwe pale. Yawe, Mungu wenu, aliwachagua wamutumikie na kubariki kwa jina lake. Wao vilevile ndio wenye mamlaka ya kuamua magomvi na maneno juu ya kuumizana.