Deuteronomy 21:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ee Mwenyezi-Mungu, uwasamehe watu wako wa Israeli ambao umewakomboa, usiwawekee watu wako Israeli hatia ya mauaji ya mtu asiye na hatia, ila uwasamehe hatia hiyo.’
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ee Mwenyezi Mungu, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ee Bwana, samehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ee Mwenyezi-Mungu, uwasamehe watu wako wa Israeli ambao umewakomboa, usiwawekee watu wako Israeli hatia ya mauaji ya mtu asiye na hatia, ila uwasamehe hatia hiyo.’
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ee BWANA, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli, ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ee bwana, ukubali upatanisho kwa watu wako Israeli, ambao umewakomboa, wala usiwahesabie watu wako hatia ya damu ya mtu asiyekuwa na hatia.” Nayo damu iliyomwagika itakuwa imefanyiwa upatanisho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ee BWANA, wasamehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ee Mwenyezi-Mungu, uwasamehe watu wako wa Israeli ambao umewakomboa, usiwawekee watu wako Israeli hatia ya mauaji ya mtu asiye na hatia, ila uwasamehe hatia hiyo.’
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Bwana, wapoze walio ukoo wako wa Isiraeli, uliowakomboa, usiwalipishe damu ya mtu asiyekora manza iliyomwagwa katikati yao walio ukoo wako wa Isiraeli! Ndipo, watakapopata upozi kwa ajili ya hiyo damu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ee BWANA, samehe watu wako Israeli, uliowakomboa, wala usiache damu ya asiye makosa ikakaa katikati ya watu wako Israeli. Na ile damu utasamehewa kwao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ee Yawe, uwasamehe watu wako wa Israeli ambao umewakomboa, usiwawekee watu wako Israeli kosa la mauaji ya mutu asiyekuwa na kosa, lakini uwasamehe kosa lile.’