Deuteronomy 22:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
watampeleka kwenye mlango wa nyumba ya baba yake na wanaume wa mji huo watampiga mawe afe, kwa sababu amefanya ufidhuli katika Israeli kwa kufanya umalaya akiwa nyumbani kwa baba yake. Ndivyo mtakavyokomesha uovu huo miongoni mwenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo wanaume wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa nyumbani mwa babaye. Lazima mwondoe uovu kati yenu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
watampeleka kwenye mlango wa nyumba ya baba yake na wanaume wa mji huo watampiga mawe afe, kwa sababu amefanya ufidhuli katika Israeli kwa kufanya umalaya akiwa nyumbani kwa baba yake. Ndivyo mtakavyokomesha uovu huo miongoni mwenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kutokuwa na utaratibu wakati akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
huyo msichana ataletwa kwenye mlango wa nyumba ya baba yake, na hapo watu wa mji wake watampiga kwa mawe hadi afe. Amefanya kitu cha aibu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa nyumbani kwa babaye. Lazima mwondoe uovu katikati yenu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na wanaume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
watampeleka kwenye mlango wa nyumba ya baba yake na wanaume wa mji huo watampiga mawe afe, kwa sababu amefanya ufidhuli katika Israeli kwa kufanya umalaya akiwa nyumbani kwa baba yake. Ndivyo mtakavyokomesha uovu huo miongoni mwenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
na wampeleke yule msichana hapo pa kuiingilia nyumba ya baba yake, hapo watu wa mji wote wampige mawe, hata afe, kwa kuwa alifanya ujinga mbaya kwao Waisiraeli wa kufanya ugoni nyumbani mwa baba yake. Hivyo ndivyo, utakavyouondoa ubaya huo katikati yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe; kwa vile alivyofanya upumbavu katika Israeli, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
watamupeleka kwenye mulango wa nyumba ya baba yake na wanaume wa muji huo watamupiga mawe akufe, kwa sababu amefanya upumbafu katika Israeli kwa kufanya ukahaba akiwa katika nyumba ya baba yake. Ndivyo mutakavyokomesha uovu huo kati yenu.