Deuteronomy 22:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Wanawake wasivae nguo za wanaume, na wanaume wasivae nguo za wanawake. Anayefanya hivyo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Haimpasi mwanamke kuvaa mavazi ya kiume wala mwanaume kuvaa mavazi ya kike, kwa maana Mwenyezi Mungu, Mungu wenu, anachukia yeyote anayefanya hivi.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Wanawake wasivae nguo za wanaume, na wanaume wasivae nguo za wanawake. Anayefanya hivyo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maana BWANA Mungu wenu anachukia ye yote ambaye hufanya hivi.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Haimpasi mwanamke kuvaa nguo za kiume wala mwanaume kuvaa nguo za kike, kwa maana bwana Mwenyezi Mungu wenu anachukia yeyote ambaye hufanya hivi.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Wanawake wasivae nguo za wanaume, na wanaume wasivae nguo za wanawake. Anayefanya hivyo ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mwanamke asivae cho chote cha mwanamume, wala mwanamume asivae nguo za kike! Kwani kila atakayefanya mambo kama hayo humchukiza Bwana Mungu wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mwanamke asivae mavazi yampasayo mwanamume, wala mwanamume asivae mavazi ya mwanamke; kwa maana kila afanyaye mambo hayo ni machukizo kwa BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Wanawake wasivae nguo za wanaume, na wanaume wasivae nguo za wanawake. Anayefanya hivyo ni chukizo kwa Yawe, Mungu wenu.