Deuteronomy 23:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kati ya vifaa vyenu mtakuwa na jembe, na hilo mtatumia kuchimba shimo na kufukia kinyesi chenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kinyesi chako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kati ya vifaa vyenu mtakuwa na jembe, na hilo mtatumia kuchimba shimo na kufukia kinyesi chenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama sehemu ya vifaa vyenu iweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama sehemu ya vifaa vyenu kuweni na kitu cha kulimia, nanyi mnapojisaidia, chimba shimo na kisha funika kile kikutokacho.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kati ya vifaa vyenu mtakuwa na jembe, na hilo mtatumia kuchimba shimo na kufukia kinyesi chenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Namo katika vyombo vyako uwe na muo; napo utakapokwenda chooni huko nje, kwanza ufukue nao kishimo, upate kukaa, kisha uyafunike yaliyokutoka.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawe uwe na jembe dogo katika silaha zako; napo uotamapo nje uchimbe kwa lile jembe, na kugeuka na kukifunika kikutokacho;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Munapaswa kuwa na pahali inje ya kambi ambapo munaweza kwenda kwa choo.