Deuteronomy 23:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Mwisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kuimiliki.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili Mwenyezi Mungu, Mungu wako, akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili Bwana, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Mwisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kuimiliki.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba BWANA Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoiingia kuimiliki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba bwana Mwenyezi Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Unaweza kutoza riba unapomkopesha mgeni, lakini ndugu yako Mwisraeli usimtoze riba, naye Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, atakubariki katika shughuli zako zote utakazofanya katika nchi ambayo unakwenda kuimiliki.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Asiye wa Kiisiraeli na umkopeshe, ujipatie faida, lakini ndugu yako usimkopeshe, ujipatie faida, kusudi Bwana Mungu wako akubarikie kazi zote, mikono yako itakazozifanya katika hiyo nchi, utakayoiingia kuichukua, iwe yako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
mgeni waweza kumkopesha kwa riba, ila usimkopeshe ndugu yako kwa riba; ili BWANA, Mungu wako, apate kukubarikia katika yote utiayo mkono wako, katika nchi uingiayo kuimiliki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Usimukopeshe ndugu yako Mwisraeli kitu kwa faida; usimulipishe faida juu ya mukopo wa feza, chakula, au chochote ambacho watu wanakopesha kwa faida.