Deuteronomy 24:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Ikiwa mwanamume ameoa mke na baadaye akawa hapendezwi naye kwa sababu ameona kwake kitu kisichofaa, basi, huyo mwanamume akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza nyumbani mwake, kisha huyo mwanamke akaondoka,
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mtu akimwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kuona jambo baya kwake, inawezekana akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani mwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Ikiwa mwanamume ameoa mke na baadaye akawa hapendezwi naye kwa sababu ameona kwake kitu kisichofaa, basi, huyo mwanamume akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza nyumbani mwake, kisha huyo mwanamke akaondoka,
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa mtu atamwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kukosa adabu, akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake,
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa mtu atamwoa mke na akamchukia kwa sababu ya kukosa adabu, naye akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza kutoka nyumbani kwake,
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni pake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Ikiwa mwanamume ameoa mke na baadaye akawa hapendezwi naye kwa sababu ameona kwake kitu kisichofaa, basi, huyo mwanamume akamwandikia hati ya talaka, akampa na kumfukuza nyumbani mwake, kisha huyo mwanamke akaondoka,
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Mtu akichukua mwanamke na kumwoa, naye halafu asipompendeza machoni pake, kwa kuwa ameona kwake neno lisilofaa, na amwandikie cheti cha kuachana na kumpa mkononi mwake, kisha na amtume kwenda zake na kutoka nyumbani mwake.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mtu akiisha kutwaa mke kwa kumwoa, asipopata kibali machoni mwake, kwa kuwa ameona neno ovu kwake, na amwandikie hati ya kumwacha, akamtilie mkononi mwake, na kumtoa katika nyumba yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Ikiwa mwanaume ameoa muke na kisha hapendezwi naye kwa sababu ameona kwake kitu kisichofaa, basi, huyo mwanaume akimwandikia barua ya kuachana, akimupa na kumufukuza kutoka katika nyumba yake, kisha huyo mwanamuke akiondoka,