Deuteronomy 25:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Tumieni mizani na vipimo vyenye uzito sahihi ili mpate kuishi maisha marefu katika nchi anayowapa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa Mwenyezi Mungu, Mungu wako.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo Bwana, Mungu wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Tumieni mizani na vipimo vyenye uzito sahihi ili mpate kuishi maisha marefu katika nchi anayowapa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa BWANA Mungu wako.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ni lazima uwe na uzito na vipimo sahihi na vya haki, ili upate kuishi maisha marefu katika nchi anayokupa bwana Mwenyezi Mungu wako.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Tumieni mizani na vipimo vyenye uzito sahihi ili mpate kuishi maisha marefu katika nchi anayowapa Mwenyezi-Mungu, Mungu wenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vyuma vyako vya kupimia sharti viwe vizima vilivyo sawasawa, nazo pishi zako ziwe nzima zilizo sawasawa, siku zako zipate kuwa nyingi katika hiyo nchi, Bwana Mungu wako atakayokupa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Uwe na jiwe timilifu la haki, uwe na kipimo kitimilifu cha haki; zipate kuwa nyingi siku zako, katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Mutumie mizani na vipimo vyenye uzito kamili na vya haki mupate kuishi maisha marefu katika inchi Yawe, Mungu wenu, anayowapa.