Deuteronomy 25:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kama ndugu wawili wa kiume wanaishi mahali fulani na mmoja wao akafariki bila kuacha mtoto wa kiume, mkewe marehemu asiolewe na mtu mwingine nje ya jamaa hiyo. Ni wajibu wa ndugu wa marehemu kumwoa mjane huyo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ikiwa ndugu wanaishi pamoja, naye mmoja wao akafa bila kuacha mwana, kamwe mjane wake asiolewe nje ya jamaa hiyo. Ndugu wa mumewe atamchukua, amwoe na kutimiza wajibu wa shemeji kwake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kama ndugu wawili wa kiume wanaishi mahali fulani na mmoja wao akafariki bila kuacha mtoto wa kiume, mkewe marehemu asiolewe na mtu mwingine nje ya jamaa hiyo. Ni wajibu wa ndugu wa marehemu kumwoa mjane huyo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao akafa bila kuacha mwana, kamwe mjane wake asiolewe nje ya jamaa hiyo. Ndugu wa mumewe atamchukua amwoe na kutimiza wajibu wa shemeji kwake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ikiwa ndugu wanaishi pamoja na mmoja wao akafa bila kuacha mwana, kamwe mjane wake asiolewe nje ya jamaa hiyo. Ndugu wa mumewe atamchukua, amwoe na kutimiza wajibu wa shemeji kwake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kama ndugu wawili wa kiume wanaishi mahali fulani na mmoja wao akafariki bila kuacha mtoto wa kiume, mkewe marehemu asiolewe na mtu mwingine nje ya jamaa hiyo. Ni wajibu wa ndugu wa marehemu kumwoa mjane huyo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndugu wakikaa pamoja, mmoja wao akafa pasipo kuacha mwana wa kiume, mkewe yule aliyekufa asiolewe nje na mtu mgeni, ila ndugu yake mumewe sharti amwingilie na kumchukua kuwa mkewe, amsimikie ndugu yake unyumba.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Watakapoketi pamoja mtu na nduguye, mmojawapo akafa, wala hana mwana wa kiume, mke wa yule aliyekufa asiolewe nje na mgeni; nduguye yule mumewe amwingilie amweke kwake awe mkewe, kumfanyia yampasayo nduguye mumewe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
“Kama wandugu wanaishi pahali fulani na mumoja wao akikufa bila kuacha mutoto mwanaume, muke wa marehemu asiolewe na mutu mwingine inje ya jamaa hiyo. Yule ndugu wa marehemu anapaswa kumwoa mujane huyo.