Deuteronomy 26:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kila baada ya miaka mitatu, kila mmoja wenu atatoa sehemu moja ya kumi ya mazao yake yote kwa ajili ya Walawi na wageni, yatima na wajane, ili wapate chakula chote wanachohitaji wanapokuwa katika miji yenu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kila baada ya miaka mitatu, kila mmoja wenu atatoa sehemu moja ya kumi ya mazao yake yote kwa ajili ya Walawi na wageni, yatima na wajane, ili wapate chakula chote wanachohitaji wanapokuwa katika miji yenu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati utakapokuwa umeshatoa zaka zote za mazao yako katika mwaka wa tatu, ambao ni mwaka wa zaka, utampa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, ili waweze kula katika miji yenu na kushiba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za mavuno yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kila baada ya miaka mitatu, kila mmoja wenu atatoa sehemu moja ya kumi ya mazao yake yote kwa ajili ya Walawi na wageni, yatima na wajane, ili wapate chakula chote wanachohitaji wanapokuwa katika miji yenu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Katika mwaka wa tatu, ndio mwaka wa kutolea mafungu ya kumi, utakapokwisha kuyatoa mafungu ya kumi yote ya mapato yako, umpe Mlawi na mgeni na mwana aliyefiwa na wazazi na mjane, wayale malangoni pako, hata washibe.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Utakapokwisha kutoa zaka, katika zaka zote za maongeo yako mwaka wa tatu, ambao ndio mwaka wa kutolea zaka, umpe zile zaka Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, wapate kula ndani ya malango yako na kushiba;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kila nyuma ya miaka mitatu, kila mumoja wenu atatoa sehemu ya kumi ya mazao yake yote kwa ajili ya Walawi na wageni, wayatima na wajane, kusudi wapate chakula chote wanachohitaji wanapokuwa katika miji yenu.