Deuteronomy 26:13 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kisha utasema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, hivi: ‘Nimelitoa nyumbani kwangu fungu takatifu, nikawapa Walawi, wageni, yatima na wajane, kama ulivyoniamuru nifanye. Sijavunja amri zako wala sijasahau.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kisha umwambie Mwenyezi Mungu, Mungu wako: “Nimeondoa katika nyumba yangu ile sehemu iliyowekwa wakfu na nimempa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, kulingana na yote uliyoamuru. Sijazihalifu amri zako wala kusahau hata mojawapo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
nawe sema mbele ya Bwana, Mungu wako, Vitu vilivyo vitakatifu nimeviondoa katika nyumba yangu, nami mimewapa Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, kwa mfano wa maagizo yako uliyoniusia yote; sikukosa maagizo yako yo yote, wala sikuyasahau;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kisha utasema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, hivi: ‘Nimelitoa nyumbani kwangu fungu takatifu, nikawapa Walawi, wageni, yatima na wajane, kama ulivyoniamuru nifanye. Sijavunja amri zako wala sijasahau.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kisha umwambie BWANA Mungu wako: “Nimeondoa katika nyumba yangu ile sehemu iliyowekwa wakfu na nimempa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, kulingana na yote uliyoamuru. Sijazihalifu amri zako wala kusahau hata mojawapo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kisha umwambie bwana Mwenyezi Mungu wako: “Nimeondoa katika nyumba yangu ile sehemu iliyowekwa wakfu na nimempa Mlawi, mgeni, yatima na mjane, kulingana na yote uliyoamuru. Sijazihalifu amri zako wala kusahau hata mojawapo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
nawe sema mbele za BWANA, Mungu wako, Vitu vilivyo vitakatifu nimeviondoa katika nyumba yangu, nami mimewapa Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, kwa mfano wa maagizo yako uliyoniusia yote; sikukosa maagizo yako yoyote, wala sikuyasahau;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kisha utasema mbele ya Mwenyezi-Mungu, Mungu wako, hivi: ‘Nimelitoa nyumbani kwangu fungu takatifu, nikawapa Walawi, wageni, yatima na wajane, kama ulivyoniamuru nifanye. Sijavunja amri zako wala sijasahau.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kisha useme mbele ya Bwana Mungu wako: Nimeyaondoa nyumbani mwangu yaliyo matakatifu, nikampa Mlawi na mgeni na mwana aliyefiwa na wazazi na mjane, nikayafanya maagizo yako yote sawasawa, kama ulivyoniagiza, sikupita agizo lako lo lote, wala sikusahau mojawapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
nawe sema mbele ya BWANA, Mungu wako, Vitu vilivyo vitakatifu nimeviondoa katika nyumba yangu, nami mimewapa Mlawi, na mgeni, na yatima, na mjane, kwa mfano wa maagizo yako uliyoniusia yote; sikukosa maagizo yako yo yote, wala sikuyasahau;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha utasema mbele ya Yawe, Mungu wako, hivi: ‘Nimetoa katika nyumba yangu fungu takatifu, nikawapa Walawi, wageni, wayatima na wajane, kama vile ulivyoniamuru nifanye. Sijavunja amri zako wala sijasahau.