Deuteronomy 26:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikula zaka yoyote nilipokuwa ninaomboleza; sikuitoa nje ya nyumba yangu nilipokuwa najisi na sikutoa zaka hiyo kwa wafu. Nimekutii ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoamuru.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sijala sehemu iliyowekwa wakfu wakati nilipokuwa nikiomboleza, wala sijaondoa mojawapo wakati nilipokuwa najisi, wala sijatoa sehemu yake yoyote kwa wafu. Nimemtii Mwenyezi Mungu, Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoniamuru.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya Bwana, Mungu wangu, nimeisikiza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikula zaka yoyote nilipokuwa ninaomboleza; sikuitoa nje ya nyumba yangu nilipokuwa najisi na sikutoa zaka hiyo kwa wafu. Nimekutii ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoamuru.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sijala sehemu iliyowekwa wakfu wakati nilipokuwa nikiomboleza, wala sijaondoa mojawapo wakati nilipokuwa najisi, wala sijatoa sehemu yake yo yote kwa wafu. Nimemtii BWANA Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoniamuru.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sijala sehemu iliyowekwa wakfu wakati nilipokuwa nikiomboleza, wala sijaondoa mojawapo wakati nilipokuwa najisi, wala sijatoa sehemu yake yoyote kwa wafu. Nimemtii bwana Mwenyezi Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoniamuru.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya BWANA, Mungu wangu, nimeisikiliza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikula zaka yoyote nilipokuwa ninaomboleza; sikuitoa nje ya nyumba yangu nilipokuwa najisi na sikutoa zaka hiyo kwa wafu. Nimekutii ee Mwenyezi-Mungu, Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoamuru.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nilipolala tanga sikuyala hata kidogo, wala nilipokuwa mwenye uchafu sikuyaondoa hata kidogo, wala sikutoa mengine kumpa mwenzangu aliyefiwa, ila nimeisikia sauti ya Bwana Mungu wangu, nikayafanya yote, kama ulivyoniagiza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
katika vitu hivyo sikula wakati wa kukaa matanga mimi, wala sikuviondoa nikiwa na unajisi, wala sikutoa kwa ajili ya wafu katika vitu hivyo; sauti ya BWANA, Mungu wangu, nimeisikiza, nimefanya yote, kama ulivyoniamuru.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sikukula sehemu ya kumi yoyote nilipokuwa ninaomboleza; sikuitoa inje ya nyumba yangu nilipokuwa muchafu na sikutoa sehemu ya kumi hiyo kwa wafu. Nimekutii ee Yawe, Mungu wangu; nimefanya kila kitu ulichoamuru juu ya sehemu ya kumi.